TIOB YATOA MAFUNZO YA UCHAMBUZI KATIKA UTOAJI MIKOPO MTANDAONI

Na Patrick Mususa, Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB

Published: 14/Jan/2019

 

Mfumo wa Utoaji Mikopo umekuwa ukipitia changamoto mbalimbali zikiwa ni pamoja na ongezeko la mikopo chechefu; kanuni mpya za kimataifa za uandaaji wa vitabu vya mahesabu yaani International Financial Reporting Standards (IFRS) vya mabenki na taasisi za fedha. Changamoto hizi zimechangia katika kupunguza utoaji wa mikopo kwa sababu za msingi za kibiashara. Kwani haiwezekani kutoa mikopo kwa wateja wenye desturi ya kutokulipa madeni yao kwa wakati.

 

Vile vile kumezidi kuwa na wito kwa mabenki kujenga na kuboresha ufahamu wa uwezo wa wateja wao kuimudu mikopo wanayopewa na kuweza kufanya hivi kupitia Mfumo sahihi wa Utoaji Mikopo.

 

Soko la Mikopo Tanzania

Ili kuelewa umuhimu wa mfumo wa Utoaji Mikopo ni vizuri kufahamu Idadi ya Mikopo yote ya ndani ya nchi (yaani Domestic Assets) kama sehemu ya uchumi wetu.

 

Kwa taarifa za Benki Kuu hadi kufikia Juni mwaka 2018 Idadi ya mikopo ya ndani na hususani iliyotolewa kwa sekta binafsi ilifikia zaidi ya Shilingi Trilioni 17.5. Hii ni zaidi ya asilimia 14% ya pato la taifa la mwaka 2017 ambalo lilifika zaidi ya Shilingi Trilioni 119.

 

Ili kulinganisha Idadi ya Mikopo ya Shilingi Trilioni 17.5 na Soko la Hisa inabidi tuangalie Idadi ya Mitaji yote iliyotolewa na wawekezaji ili kununua Hisa katika soko letu la DSE. Na kwa mujibu wa ripoti ya soko la hisa ya Ijumaa tarehe 11 Januari 2019 Idadi ya Mtaji wa soko zima la hisa la DSE ilifikia Shilingi Trilioni 19.2 Idadi hii ikiwa pia ni thamani ya makampuni yote 28 ambayo yameorodheshwa Ubaoni DSE. Hii inaonyesha kwamba idadi jumla ya mikopo ambayo imekwisha tolewa kwa wafanyabiashara, makampuni pamoja na watu binafsi inafikia asilimia 91% ya ukubwa wa soko la hisa DSE.

 

Kutokana na ukubwa wa soko la mikopo nchini Tanzania, mbinu za uchambuzi zinazotumika na watendaji wafanyakazi wa taasisi za kifedha zinapaswa kuwa mbinu zenye viwango stahiki ili kuhakikisha kwamba uchambuzi yakinifu unafanyika kabla ya mikopo kutolewa. Kwani athari kwa uchumi wa nchi zitakuwa kubwa zaidi endapo mikopo chechefu itaendelea kuongezeka sambamba na utoaji wa mikopo mipya.

 

TIOB, ikiwa ni kati ya wadau wakuu wa maendeleo ya sekta ya fedha nchini, imekuwa ikitoa huduma ya Mafunzo ya muda mfupi yaani “Continuous Professional Development” na ya muda mfrefu kwa upande wa taaluma yaani “Certfied Profesional Banking Certificates” kwa wafanyakazi wa mabenki na taasisi nyingine za fedha nchini kwa kipindi cha zaidi ya miaka 25. Wafanyakazi wa taasisi mbali mbali za fedha wamekuwa wakipitia mfumo wa masomo na mitihani ya TIOB ili kujijenga kitaaluma kama “Bankers” au “Watoa Huduma ya Fedha” katika sekta.

 

Uzinduzi wa Kozi ya Uchambuzi wa Mikopo

Katika juhudi za kuitikia wito wa wadau mbali mbali na kukidhi mahitaji ya sekta ya fedha nchini, TIOB imefungua mwaka huu 2019 kwa kuzindua kozi mpya ya “UCHAMBUZI YAKINIFU KUPITIA VIASHIRIA HATARISHI KATIKA MFUMO WA UTOAJI MIKOPO” yaani “CREDIT RISK MODELLING”.

Kozi hii mpya imeandaliwa kwa kushirikiana na kampuni ya Marekani ya KENTARA ANALYTICS iliyobobea katika masuala ya Uchambuzi Yakinifu wa Biashara na Fedha pamoja na Masomo kwa njia ya Mtandao.

 

Hivyo kozi hii mpya itapatikana kwa njia ya mtandao ili kurahisisha upatikanaji wake kwa wadau wote wa sekta ya fedha. Msomaji anapotaka kujiunga na kozi hii ya “CREDIT RISK MODELLING” anapaswa kwenda https://tiob.teachable.com na kukamilisha usajili wake. Baada ya hili msomaji anapaswa kufanya malipo stahiki ya kozi hiyo kwa kutuma kiasi cha pesa kilichowekwa kwenye taarifa za kozi kwenda kwenye akaunti ya benki ya TIOB ya NMB 20110028061 au STANBIC 9120000365163 aidha kupitia kwa Wakala; M-Pesa; au Tigopesa. Baada ya malipo msomaji anapaswa kutuma kivuli cha risiti ya malipo au kuituma ujumbe was simu wa uhakiki wa malipo kwa njia ya barua pepe kwenda training@tiob.or.tz ili kupatiwa coupon au vocha ya kuifungua kozi yake kwenye mtandao na kuendelea na masomo.

 

Kozi hii inatarajiwa kuwa na mafunzo yanayoeleweka kwa urahisi kwa mtumishi au mfanyakazi yeyote katika sekta ya fedha, kuanzia karani katika kitengo cha huduma kwa wateja hadi mkuu wa idara ya mikopo. Mafunzo haya yameandaliwa kwa njia ya maandishi pamoja na video na sauti zilizorekodiwa. Vile vile kozi hii itakuwa inatoa vyeti kwa wahitimu kwa njia ya dijitali, vyeti ambavyo vinaweza kuhifadhiwa kielektroniki au kutolewa kwenye printer kama nakala ya mkononi (au hard copy).

 

Usajili na Uwanachama

Si haba kwamba hadi leo TIOB imesajili zaidi ya wanachama (yaani members) elfu 7,000 ambao ni zaidi ya asilimia 50% ya wafanyakazi wote wa mabenki chini. Taasisi ya TIOB inayo matumaini makubwa kwamba mfumo wake wa kiTeknohama wa Usajili wa Wanachama (yaani SARIS) utazidi kupokea wanachama wapya wengi zaidi baada ya uzinduzi wa kozi hii. Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama wa TIOB kwa kupitia njia mbili: Uwanachama chini ya Ajira katika Benki (Ordinary Membership); au Uwanachama Binafsi (Student Membership).

 

Mwanachama anapohitimu mitihani ya TIOB katika ngazi ya juu ya taaluma ya kibenki yaani “Professinal Banking” hupanda ngazi na kuwa “Associate Member” au “Mwanachama Mshirika” wa TIOB.

 

Kozi hii mpya ya TIOB ya “CREDIT RISK MODELLING” ikiwa imeandaliwa kwa kuwalenga watendaji katika mfumo wa Utoaji Mikopo, imewavutia pia washiriki kutoka nje ya sekta ya Fedha, wengi wao wakitamani kujifahamisha zaidi jinsi maombi ya mikopo inavyochambuliwa na kufanyiwa utathmini na mwishowe kupitishwa au kukataliwa.

 

Kozi ya “CREDIT RISK MODELLING” inapatikana katika tovuti ya https://tiob.teachable.com na usajili umeshaanza. Bei za vipindi ni Tshs 30,000 kwa kozi nzima na Tshs 20,000 kwa kila kipengele kati ya vipengele viwili vya “Analyst Track” na “Non-Analyst Track”.